APRM Tanzania na UONGOZI Institute kujadili maeneo ya ushirikiano
APRM Tanzania na UONGOZI Institute wamefanya kikao kazi kwa lengo la kujadili na kubainisha maeneo ya ushirikiano kati ya taasisi hizo, hususan katika kuimarisha uongozi na utawala bora.
Kikao hicho pia kilijikita katika namna ya kutumia utaalamu na uzoefu wa taasisi hizo katika kujenga uwezo, kuimarisha utendaji wa viongozi na taasisi, pamoja na kuchochea mijadala ya kisera yenye tija kwa maendeleo ya Taifa.
Ushirikiano huo unatarajiwa kufungua fursa zaidi za mafunzo, mijadala ya sera na kubadilishana maarifa na uzoefu, kwa lengo la kuongeza thamani na kuleta matokeo chanya katika uongozi na utawala nchini.
#APRM Tanzania #UONGOZIInstitute #Leadership #GoodGovernance #Tanzania





