APRM TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA PILI WA MWAKA UNAOHUSU MAENDELEO YA MASOKO YA MITAJI BARANI AFRIKA NA UZINDUZI WA AfCRA
Mauritius | Oktoba 2026
APRM Tanzania imeshiriki katika mkutano muhimu uliojadili maendeleo ya masoko ya mitaji barani Afrika, sambamba na uzinduzi wa Africa Credit Rating Agency (AfCRA).
AfCRA ni Taasisi ya Afrika inayolenga kutoa tathmini za uwezo wa nchi kukopesheka zinazozingatia mazingira halisi ya kiuchumi ya Afrika.
Taasisi hii inalenga kuimarisha uwazi na uelewa wa uchumi wa Afrika, kujenga imani kwa wawekezaji, kukuza masoko ya mitaji na fursa za uwekezaji pamoja na kuchangia juhudi za Afrika kugharamia maendeleo yake endelevu.
Kwa Tanzania, hatua hii inatoa fursa ya kuendeleza mwonekano chanya wa uwezo wa uchumi wetu na kuvutia uwekezaji unaochochea maendeleo.

_1016_652shar-30brig-10.jpeg)


