APRM TANZANIA YAIPONGEZA SERIKALI KWA SERA MPYA ZA MAENDELEO ENDELEVU YA VIWANDA NA SERA YA MAENDELEO YA JASIRIAMALI NDOGO NA ZA KATI (SMEs)
APRM inaipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuzindua Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda ya mwaka 2025 na Sera iliyoboreshwa ya Maendeleo ya Jasiriamali ndogo na za kati (SMEs) ya mwaka 2003, Toleo la mwaka 2025.
Uzinduzi wa Sera hizi unaashiria hatua muhimu katika jitihada za nchi kuimarisha maendeleo endelevu ya viwanda, mageuzi ya kiuchumi na maendeleo jumuishi pamoja na kuweka msisitizo katika kuimarisha uwezo wa uzalishaji wa ndani, kukuza ujasiriamali, kuongeza thamani ya rasilimali zinazozalishwa nchini na kujenga mazingira wezeshi kwa biashara kukua na kushindana katika uchumi wa kikanda na kimataifa.
Kupitia Sera hizi, Tanzania inawekeza kwa watu wake kwa; kuwezesha biashara ndogo na za kati; kukuza viwanda na kuongeza thamani za bidhaa; kupanua fursa: kuimarisha biashara nchini, kikanda na bara ikiwemo ushiriki wa biashara huria ya Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA) na kutengeneza ajira jambo ambalo ni nguzo muhimu ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050 (Dira 2050) na matarajio ya maendeleo ya kikanda na bara la Afrika.
Mafanikio haya yanaonesha uhusiano wa karibu kati ya mageuzi ya kiuchumi na Utawala Bora, kwani kufikiwa kwa maendeleo yaliyokusudiwa kupitia matokeo ya viwanda na biashara kunahitaji taasisi imara, uratibu madhubuti wa kisera, uwazi, uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau mbalimbali.
_500_500shar-50brig-20_c1.jpeg)

