APRM INAENDELEA KUWA CHOMBO MUHIMU CHA KUIMARISHA UTAWALA BORA
Katibu Mtendaji wa African Peer Review Mechanism (APRM) Tanzania, Bw. Lamau Mpolo, amesema kuwa APRM inaendelea kuwa chombo muhimu katika kuimarisha utawala bora, uwajibikaji na maendeleo endelevu barani Afrika. Amesema kupitia mfumo wa tathmini ya hiari kati ya nchi wanachama, mataifa hupata fursa ya kujitathmini katika masuala ya utawala wa kisiasa, uchumi na maendeleo ya kijamii ili kubaini changamoto na kuweka mikakati ya maboresho.
Lamau Mpolo ameeleza kuwa kupitia mchakato wa African Peer Review Mechanism, kumekuwa na ongezeko la uelewa kuhusu umuhimu wa uwazi, ushirikishwaji wa wananchi na uwajibikaji wa viongozi. Amesema hatua hiyo imechangia kuimarisha taasisi za umma na kusaidia nchi za Afrika kujifunza uzoefu na mbinu bora kutoka kwa wenzao ili kufikia maendeleo endelevu.
_1016_1016shar-30brig-10.jpeg)


