Wabobezi katika masuala mbali mbali nchini (Technical Assessment Team) wameombwa kuwa tayari kuanza mchakato wa kufanya tathmini ya pili ya Utawala Bora Nchini ambapo itahusisha maeneo Demokrasia na Utawala wa Kisiasa, Usimamizi wa Uchumi, Utendaji wa Mashirika ya biashara na Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi.