Maridhiano ni uwekezaji katika utawala bora, amani na mshikamano wa kimataifa. APRM Tanzania inaamini kuwa mazungumzo ya kujenga maridhiano, ushirikishwaji wa wadau na utekelezaji wa makubaliano ni miongoni mwa misingi muhimu ya utawala bora, amani na maendeleo endelevu. Maridhiano kama haya ni msingi wa kujenga Tanzania imara, uchumi imara na mustakabali wenye matumaini zaidi kwa vizazi vijavyo.

Pichani ni Utiaji saini wa ajenda zilizokubaliwa na pande zote mbili kwa ajili ya kufanyiwa kazi kufuatia Tamko la Pamoja la Muafaka wa Kisiasa Zanzibar kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ACT-Wazalendo.