Uongozi wa APRM Tanzania na APRM Namibia umekutana na kufanya mazungumzo katika kikao cha pamoja cha kubadilishana uzoefu kilichofanyika Widhoek nchini Namibia. Kikao hicho kilikuwa na lengo la kuangalia muundo wa Baraza la Usimamazi la Taifa (NGC),muundo wa Menejimenti, njia zinazotumika kutafuta rasilimali fedha pamoja na kutambua mikakati inayotumika katika kufanya utekelezaji wa mpango wa Taifa wa Ripoti za APRM (National Program of Action). Masuala mbalimbali yalizungumzwa katika kikao hicho ambayo yanalenga kushajihisha utawala bora ndani ya Africa pamoja na kusukuma mbele Agenda ya 2063. Viongozi walioshiriki katika kikao hicho ni Mtendaji Mkuu wa APRM Namibia Balozi Lineekela Mboti, Mwenyekiti wa NGC Namibia Balozi Wilried Emvula, Balozi wa Tanzania Nchini Namibia Bal Ceasor Waitara, Katibu Mtendaji APRM Tanzania Bw. Lamau Mpolo na watendaji wengine kutoka APRM Namibia na Tanzania. #utawalaborakwamaendeleoendelevu #utawala