Uongozi mpya wa Taasisi ya mpango wa hiari wa Tathimini ya Utawala Bora Barani Afrika (APRM Tanzania) iliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki umetambulishwa rasmi kwa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania(TPSF).

Zoezi hilo limefanywa na Katibu Mtendaji wa APRM Tanzania Bwana Lamau Mpolo mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bwana Raphael Maganga katika mkutano mfupi uliofanyika katika ofisi za TPSF jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, Taasisi hizo zimekubaliana mambo mbalimbali ikiwemo kuimarisha mahusiano, kubadirishana uzoefu na kuhamasisha ushirikishwaji wa Sekta Binafsi katika Utawala Bora hususani katika kipindi hiki kuelekea kutengeneza ripoti ya pili ya tathimini ya Serikali ya utawala bora hapa nchini.