Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Slovakia zimethibitisha dhamira ya kuimarisha uhusiano ya kidiplomasia, ushirikiano wa kiuchumi, uwekezaji, pamoja na kubadilishana uzoefu wa kiutamaduni kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.
Hayo yamesemwa Juni 11,2026 wakati wa Jukwaa la Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Tanzania na Slovakia lililowakutanisha wawekezaji, viongozi wa biashara, wajasiriamali na wawakilishi wa serikali jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo lilitoa fursa ya kujadili maeneo mapya ya ushirikiano na kukuza ukuaji wa uchumi endelevu na kubadilishana mawazo kuhusu namna ya kuongeza biashara, uwekezaji na ushirikiano katika sekta mbalimbali muhimu kwa maendeleo ya nchi hizo mbili.
Akizungumza katika jukwaa hilo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, alisema jukwaa hilo ni fursa ya kipekee ya kujenga ushirikiano.

Naye, Waziri wa Mambo ya Nje na Masuala ya Ulaya wa Slovakia, Mhe. Juraj Blanár, alisema Slovakia inaiona Tanzania kama mshirika wa kimkakati na si soko pekee na kusisitiza utayari wao kuimarisha ushirikiano
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)