Wadau mbalimbali akiwemo Balozi wa Korea Kusini Mheshimiwa KIM SP, jopo la wanafunzi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar waliotembelea banda la maonesho la APRM Tanzania katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam ikiwa ni maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa walipata fursa ya kujifunza utendaji kazi wa APRM pamoja na mikakati ya maandalizi ya Ripoti ya Pili ya Tathimini ya Utawala Bora Tanzania.
