APRM ni kifupi cha African Peer Review Mechanism, ambapo ni Taasisi mojawapo za Umoja wa Mataifa (AU) na ni mpango wa hiyari wa kujipima na kujithamini kwa vigezo vya Utawala Bora APRM ni Taasisi ambayo inafanya kazi zake chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Taasisi hii kazi yake ni kuratibu mpango wa hiyari ambao unahusisha Nchi huru za Africa kujitathimini zenyewe kwa vigezo vya Utawala Bora. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliteuliwa kuwa Wizara unganishi kati ya Serikali ya Jamhuri ya Tanzania-APRM Tanzania na Makao Makuu ya APRM yaliyoko Afrika ya Kusini.
https://www.instagram.com/reel/C3kV_MnNs_E/?igsh=MTc4MmM1YmI2Ng==
Lengo ni Nchi huru za Afrika zenye uwezo wa kujipima na kuweza kujitathmini zenyewe baada ya kufanya shughuli zake za maendeleo kuona zimefanikiwa kiasi gani. APRM Tanzania ilifanikiwa kutoa ripoti ya kwanza ya Tathmini na ilikamilika mwaka 2013 na kuwasilishwa mwaka 2017, ilizinduliwa na aliyekuwa Makamu wa Rais Dkt. Samila Suluhu Hassan ambaye sasa hivi ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ripoti ile ilikuwa na mazuri mengi ikiwa ni pamoja na Tanzania kuwa kinara katika masuala ya Utawala Bora kutokana na kuingia kwa Amani katika mfumo wa vyama vingi, mfumo wa kupokezana madaraka ya Urais na suala la Muungano ambalo sio Kivutio kwa Afrika tu lakini ni kivutio kwa Dunia nzima, jambo jingine ni suala la lugha yetu ya Kiswahili, tunasema Tanzania kuna makabila zaidi ya 120 lakini sote tunaunganishwa na lugha ya Kiswahili na jambo jingine ni kuwasilishwa kwa ripoti za Mkaguzi wa Serikali kwa Uwazi Wapi kuna shida na wapi ziweze kuboresha ili ziweze kusonga mbele. Tathmini tunazozifanya sio tu kuangalia mafanikio ya Serikali, tunachokifanya ni kuangazia mafanikio lakini pia tunaangazia maeneno mengine yenye changamoto na kuziibua ili Serikali iweze kuzitambua. Kwahiyo wanatakiwa wakitumie hiki chombo kwaajili ya kuzungumza yale yaliyopo katika jamii ili Serikiali iweze kutatua lakini pale inapofanya vizuri yaweze kuongezewa nuru. Chombo hiki ni chombo kizuri sana kwani hatuwashirikishi tu kwenye kupata mawazo lakini kwenye Baraza la Usimamamizi wa APRM linatokana na Wanajamii na Wawakilishi kutoka makundi mbalimbali, Vvyama Vya siasa, Serikali zote mbili na Makundi Maalumu, vijana, walemavu, Wakina Mama wanawakilishwa.
