APRM Tanzania tunapenda kutoa Pongezi na Hongera kwa Mhe. Balozi Marie-Antoinette Rose Quatre kwa kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa APRM Bara. Balozi Rose Quatre, Raia wa Seychelles, analeta uzoefu mkubwa kwa APRM, ikiwa ni pamoja na kuhudumu kama Balozi wa Nchi kadhaa Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU), Mbunge, na Kiongozi wa Shughuli za Serikali katika Bunge la Kitaifa la Seychelles. Uzoefu wake na uongozi bora bila shaka utachangia katika kuendelea kwa mafanikio na ukuaji wa APRM. Karibu kwenye Familia ya APRM.