Dar es salaam
African Peer Review Mechanism (APRM Tanzania) imekuatana na shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na tathmini ya Utawala Bora hususani katika kuelekea maandalizi ya Ripoti ya Pili ya APRM Tanzania itakayogusa maeneo ya Demokrasia na Utawala wa siasa, Usimamizi wa Uchumi na mashirika ya Biashara na Maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Katika kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi za UNDP zilizopo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa APRM Tanzania Lamau Mpolo alielezea juu ya mpango wa hiari wa kujitathimini na kusema kuwa tayari APRM imeshakamilisha hatua ya kukutana na Wataalamu wabobezi pamoja na kuandaa hojaji ambazo zitatumika katika tathmini hiyo.
Aidha amesema kuwa APRM inalishukuru sana Shirika la UNDP kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo na kusisistiza kuwa nguvu kubwa waloiweka katika APRM ilisababisha Ripoti ya kwanza kuweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa hivyo ameiomba UNDP kuendelea kuiunga mkono kwa kuendeleza mashirikiano yaliopo.
Akizungumza katika mkutano huo Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa Christine Mwasisi amesema kuwa UNDP itaendelea kuwa mshirika mzuri wa maendeleo kwa Tanzania na kutoa ushirikiano katika kutekeleza miradi mbalimbali na kuwaomba uongozi wa APRM kuhakikisha inawashirikisha wananchi katika kutoa maoni yao ili lengo la APRM kuwa sauti ya wananchi liweze kutimia.





